12. Wakasafiri kutoka nyika ya Sini, wakapanga Dofka.
13. Wakasafiri kutoka Dofka, wakapanga Alushi.
14. Wakasafiri kutoka Alushi, wakapanga Refidimu, ambapo hapakuwa na maji ya watu kunywa.
15. Wakasafiri kutoka Refidimu, wakapanga katika nyika ya Sinai.
16. Wakasafiri kutoka nyika ya Sinai, wakapanga Kibroth-hataava.
17. Wakasafiri kutoka Kibroth-hataava, wakapanga Haserothi.
18. Wakasafiri kutoka Haserothi, wakapanga Rithma.
19. Wakasafiri kutoka Rithma, wakapanga Rimon-peresi.
20. Wakasafiri kutoka Rimon-peresi, wakapanga Libna.
21. Wakasafiri kutoka Libna, wakapanga Risa.
22. Wakasafiri kutoka Risa, wakapanga Keheletha.
23. Wakasafiri kutoka Keheletha, wakapanga katika mlima wa Sheferi