27. lakini sisi watumishi wako tutavuka, kila mume aliyevaa silaha za vita, mbele za BWANA, tuende vitani, kama wewe bwana wangu usemavyo.
28. Basi Musa akamwagiza Eleazari kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni, na wakuu wa nyumba za mababa za kabila za wana wa Israeli, katika habari za watu hao.
29. Musa akawaambia, Kwamba wana wa Gadi, na wana wa Reubeni, watavuka Yordani pamoja nanyi, kila mtu aliyevaa silaha kwa vita, mbele za BWANA, nayo nchi itashindwa mbele yenu; ndipo mtawapa nchi ya Gileadi kuwa milki yao;
30. lakini ikiwa hawataki kuvuka pamoja nanyi, hali wamevaa silaha zao, ndipo watakuwa na milki zao kati yenu katika nchi ya Kanaani.
31. Wana wa Gadi, na wana wa Reubeni, wakajibu na kusema, Kama BWANA alivyotuambia sisi watumishi wako, ndivyo tutakavyofanya.
32. Tutavuka, hali tumevaa silaha zetu, mbele za BWANA, kuingia nchi ya Kanaani, nayo milki ya urithi wetu itakuwa ng’ambo ya pili ya Yordani.
33. Basi Musa akawapa wao, maana, wana wa Gadi, na wana wa Reubeni, na hiyo nusu ya kabila ya Manase, mwana wa Yusufu, ufalme wa Sihoni mfalme wa Waamori, na ufalme wa Ogu mfalme wa Bashani, hiyo nchi, kama miji yao ilivyokuwa, pamoja na mipaka yake, maana, miji ya hiyo nchi iliyozunguka kotekote.
34. Kisha wana wa Gadi wakajenga Diboni, na Atarothi, na Aroeri;
35. na Atrothi-shofani, na Yazeri, na Yogbeha;
36. na, Beth-nimra, na Beth-harani; miji yenye maboma, na mazizi ya kondoo.
37. Na wana wa Reubeni wakajenga Heshboni, na Eleale, na Kiriathaimu;
38. na Nebo, na Baal-meoni, (majina yake yalikuwa yamegeuzwa) na Sibma; nao wakaiita miji waliyoijenga majina mengine.
39. Na wana wa Makiri mwana wa Manase wakaenda Gileadi, na kuitwaa, na kuwapokonya Waamori waliokuwamo humo.
40. Basi Musa akampa Makiri, mwana wa Manase, Gileadi, naye akakaa humo.
41. Kisha Yairi mwana wa Manase akaenda na kuvitwaa vijiji vya Gileadi. Akaviita jina lake Hawoth-yairi.