49. wakamwambia Musa wakisema, Sisi watumishi wako tumefanya jumla ya hesabu ya watu wa vita walio chini ya mikono yetu, na hapana hata mmoja aliyetupungukia.
50. Nasi tumeleta matoleo ya BWANA, aliyopata kila mtu, ya vyombo vya dhahabu, na mitali, na timbi, na pete za muhuri, na vipini, na vikuku, ili kuzifanyia upatanisho nafsi zetu mbele ya BWANA.
51. Musa na Eleazari kuhani wakapokea kwao hiyo dhahabu, maana, vile vyombo vyote vilivyofanyizwa.
52. Na dhahabu yote ya sadaka ya kuinuliwa waliyosongeza kwa BWANA, ya maakida wa elfu elfu, na maakida wa mia mia, ilikuwa shekeli kumi na sita elfu na mia saba na hamsini.
53. (Kwa kuwa hao watu wa vita walikuwa wametwaa nyara, kila mtu nafsi yake.)
54. Basi Musa na Eleazari kuhani wakapokea hiyo dhahabu mikononi mwa hao maakida wa elfu elfu na wa mia mia, na kuileta ndani ya hema ya kukutania, ili iwe ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli mbele za BWANA.