1. Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
2. Walipize kisasi wana wa Israeli juu ya Wamidiani; kisha baadaye utakusanywa uwe pamoja na watu wako.
3. Basi Musa akanena na watu, na kuwaambia, Wavikeni silaha watu miongoni mwenu waende vitani, ili waende kupigana na Midiani, wapate kumlipiza kisasi BWANA, juu ya Midiani.
4. Katika kila kabila mtatoa watu elfu, katika kabila zote za Israeli, nanyi mtawapeleka waende vitani.
5. Basi walitolewa katika maelfu ya Israeli, elfu moja ya kila kabila, watu waume kumi na mbili elfu walioandaliwa kwa vita.
6. Basi Musa akawapeleka, watu elfu wa kila kabila waende vitani, wao na Finehasi mwana wa Eleazari kuhani, waende vitani, na vile vyombo vya mahali patakatifu, na hizo tarumbeta za kupiga sauti za kugutusha mkononi mwake.