16. Tena, mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, ni pasaka ya BWANA.
17. Siku ya kumi na tano ya mwezi huo patakuwa na sikukuu; mkate usiotiwa chachu utaliwa muda wa siku saba.
18. Siku ya kwanza patakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi;
19. lakini mtaisongeza sadaka kwa njia ya moto, sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA; ng’ombe waume wadogo wawili, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza saba; watakuwa wakamilifu kwenu;
20. pamoja na sadaka zake za unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta; mtasongeza sehemu ya kumi tatu kwa ng’ombe mmoja, na sehemu ya kumi mbili kwa kondoo mume;
21. na sehemu ya kumi moja utasongeza kwa kila mwana-kondoo, wale wana-kondoo saba;
22. tena mtasongeza mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.