Hes. 27:5-12 Swahili Union Version (SUV)

5. Basi Musa akaleta neno lao mbele ya BWANA

6. BWANA akanena na Musa, na kumwambia,

7. Hao binti za Selofehadi wananena lililo haki; kweli utawapa milki ya urithi pamoja na ndugu za baba yao; nawe utawapa urithi wa baba yao.

8. Kisha utanena na wana wa Israeli, na kuwaambia, Mtu akifa, naye hana mwana wa kiume, ndipo utampa binti yake urithi wake.

9. Tena ikiwa hana binti, mtawapa nduguze urithi wake.

10. Na ikiwa hana ndugu, mtawapa ndugu za babaye huo urithi wake.

11. Tena ikiwa babaye hana ndugu, utampa huyo aliye karibu naye katika jamaa zake huo urithi wake, naye atakuwa nao; na neno hili litakuwa ni amri ya hukumu kwa wana wa Israeli, kama BWANA alivyomwagiza Musa.

12. BWANA akamwambia Musa, Panda wewe juu ya mlima huu wa Abarimu, uitazame nchi niliyowapa wana wa Israeli.

Hes. 27