Hes. 26:41-48 Swahili Union Version (SUV)

41. Hao ndio wana wa Benyamini kwa jamaa zao; na waliohesabiwa kwao walikuwa arobaini na tano elfu na mia sita.

42. Na wana wa Dani ni hawa kwa jamaa zao; wa Shuhamu, jamaa ya Washuhamu. Hizi ndizo jamaa za Dani kwa jamaa zao.

43. Jamaa zote za Washuhamu, kama waliohesabiwa kwao, walikuwa sitini na nne elfu na mia nne.

44. Na wana wa Asheri kwa jamaa zao; wa Imna, jamaa ya Waimna; wa Ishvi jamaa ya Waishvi; wa Beria, jamaa ya Waberia.

45. Wa wana wa Beria; wa Heberi, jamaa ya Waheberi; wa Malkieli, jamaa ya Wamalkieli.

46. Na jina la binti wa Asheri aliitwa Sera.

47. Hizi ndizo jamaa za wana wa Asheri kama waliohesabiwa kwao, hamsini na tatu elfu na mia nne.

48. Na wana wa Naftali kwa jamaa zake; wa Yaseeli, jamaa ya Wayaseeli; na wa Guni, jamaa ya Waguni;

Hes. 26