31. na wa Asrieli, jamaa ya Waasrieli; na wa Shekemu, jamaa ya Washekemu;
32. na wa Shemida, jamaa ya Washemida; na wa Heferi, jamaa ya Waheferi.
33. Na Selofehadi mwana wa Heferi hakuwa na wana waume, isipokuwa wa kike; na majina ya hao binti za Selofehadi ni haya, Mala, na Noa, na Hogla, na Milka, na Tirsa.
34. Hizi ndizo jamaa za Manase; na waliohesabiwa kwao walikuwa ni hamsini na mbili elfu na mia saba.
35. Na wana wa Efraimu kwa jamaa zao; wa Shuthela, jamaa ya Washuthela; wa Beredi, jamaa ya Waberedi; wa Tahathi, jamaa ya Watahathi.
36. Na wana wa Shuthela ni hawa; wa Erani, jamaa ya Waerani.