24. wa Yashubu, jamaa ya Wayashubu; wa Shimroni, jamaa ya Washimroni.
25. Hizi ndizo jamaa za Isakari kama waliohesabiwa kwao, sitini na nne elfu na mia tatu.
26. Na wana wa Zabuloni kwa jamaa zao; wa Seredi, jamaa ya Waseredi; wa Eloni, jamaa ya Waeloni; wa Yaleeli, jamaa ya Wayaleeli.
27. Hizi ndizo jamaa za Wazabuloni kama waliohesabiwa kwao, sitini elfu na mia tano.
28. Na wana wa Yusufu kwa jamaa zao; Manase na Efraimu.