Hes. 26:17-28 Swahili Union Version (SUV)

17. wa Arodi, jamaa ya Waarodi; wa Areli, jamaa ya Waareli.

18. Hizi ndizo jamaa za wana wa Gadi kama waliohesabiwa kwao, arobaini elfu na mia tano.

19. Na wana wa Yuda, Eri na Onani; na hao Eri na Onani wakafa katika nchi ya Kanaani.

20. Na wana wa Yuda kwa jamaa zao; wa Shela, jamaa ya Washela; wa Peresi, jamaa ya Waperesi; wa Zera, jamaa ya Wazera.

21. Na wana wa Peresi walikuwa; wa Hesroni, jamaa ya Wahesroni; wa Hamuli, jamaa ya Wahamuli.

22. Hizi ndizo jamaa za Yuda kama waliohesabiwa kwao, sabini na sita elfu na mia tano.

23. Na wana wa Isakari kwa jamaa zao; wa Tola, jamaa ya Watola; wa Puva, jamaa ya Wapuva;

24. wa Yashubu, jamaa ya Wayashubu; wa Shimroni, jamaa ya Washimroni.

25. Hizi ndizo jamaa za Isakari kama waliohesabiwa kwao, sitini na nne elfu na mia tatu.

26. Na wana wa Zabuloni kwa jamaa zao; wa Seredi, jamaa ya Waseredi; wa Eloni, jamaa ya Waeloni; wa Yaleeli, jamaa ya Wayaleeli.

27. Hizi ndizo jamaa za Wazabuloni kama waliohesabiwa kwao, sitini elfu na mia tano.

28. Na wana wa Yusufu kwa jamaa zao; Manase na Efraimu.

Hes. 26