Hes. 26:1-10 Swahili Union Version (SUV)

1. Ikawa baada ya hilo pigo, BWANA akanena na Musa na Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, na kuwaambia,

2. Fanya jumla ya mkutano wote wa wana wa Israeli, tangu umri wa miaka ishirini, na zaidi, kwa nyumba za baba zao, hao wote katika Israeli wawezao kutoka kuenenda vitani.

3. Kisha Musa na Eleazari kuhani wakanena nao katika nchi tambarare za Moabu karibu na mto wa Yordani, huko Yeriko, wakawaambia,

4. Fanyeni jumla ya watu, tangu umri wa miaka ishirini, na zaidi; kama BWANA alivyomwagiza Musa na wana wa Israeli, hao waliotoka nchi ya Misri.

5. Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli, wana wa Reubeni; wa Hanoki, jamaa ya Wahanoki; na wa Palu, jamaa ya Wapalu;

6. na wa Hesroni, jamaa ya Wahesroni; na wa Karmi, jamaa ya Wakarmi.

7. Hizi ndizo jamaa za Wareubeni; na hao waliohesabiwa kwao walikuwa arobaini na tatu elfu na mia saba na thelathini.

8. Na wana wa Palu; Eliabu.

9. Na wana wa Eliabu; Nemueli, na Dathani, na Abiramu. Hawa ndio Dathani na Abiramu waliochaguliwa na mkutano, ambao walishindana na Musa na Haruni katika mkutano wa Kora, hapo waliposhindana na BWANA;

10. nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza pamoja na Kora, mkutano huo ulipokufa; wakati moto ulipowateketeza watu mia mbili na hamsini, nao wakawa ishara.

Hes. 26