27. Kisha Balaki akamwambia Balaamu, Haya, njoo sasa, nikupeleke mahali pengine; labda Mungu ataridhia kwamba unilaanie watu hao huko.
28. Basi Balaki akamchukua Balaamu akaenda naye mpaka kilele cha mlima Peori, mahali paelekeapo upande wa nyika iliyo chini yake.
29. Balaamu akamwambia Balaki, Haya, unijengee hapa madhabahu saba, kisha uniandalie ng’ombe waume saba, na kondoo waume saba.
30. Basi Balaki akafanya kama Balaamu alivyosema, akasongeza sadaka ng’ombe mume na kondoo mume juu ya kila madhabahu.