Hes. 22:39-41 Swahili Union Version (SUV)

39. Balaamu akaenda pamoja na Balaki wakafika Kiriath-husothi.

40. Balaki akachinja ng’ombe, na kondoo, akampelekea Balaamu na wale wakuu waliokuwa pamoja naye.

41. Ikawa asubuhi Balaki akamchukua Balaamu, akampandisha hata mahali pa juu pa Baali; na kutoka huko akawaona watu, hata pande zao za mwisho.

Hes. 22