Hes. 21:13-20 Swahili Union Version (SUV)

13. Kutoka huko wakasafiri, wakapanga upande wa pili wa Arnoni, ulio jangwani, utokao katika mpaka wa Waamori; maana, Arnoni ndio mpaka wa Moabu, kati ya Moabu na Waamori.

14. Kwa hiyo imesemwa katika chuo cha Vita vya BWANA,Wahebu katika Sufa,Na bonde za Arnoni,

15. Na matelemko ya hizo bondeKwenye kutelemkia maskani ya Ari,Na kutegemea mpaka wa Moabu.

16. Kutoka huko wakasafiri kwenda Beeri; ni kisima ambacho BWANA alimwambia Musa, Uwakutanishe watu, nami nitawapa maji.

17. Ndipo Israeli wakaimba wimbo huu;Bubujika Ee kisima; kiimbieni;

18. Kisima walichokichimba wakuu,Ambacho wakuu wa watu wakakifukua,Kwa fimbo za enzi, kwa fimbo zao.Kutoka lile jangwa wakaenda Matana;

19. na kutoka Matana wakaenda Nahalieli; na kutoka Nahalieli wakaenda Bamothi;

20. na kutoka Bamothi wakaenda bondeni kwenye konde la Moabu, hata kilele cha Pisga, kielekeacho chini jangwani.

Hes. 21