Hes. 2:1-8 Swahili Union Version (SUV)

1. BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,

2. Wana wa Israeli watapanga kila mtu penye beramu yake mwenyewe, na alama za nyumba za baba zao; kuikabili hema ya kukutania ndiko watakakopanga kwa kuizunguka pande zote.

3. Na hao watakaopanga upande wa mashariki, kwa kuelekea maawio ya jua, ndio wale wa beramu ya marago ya Yuda, kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Yuda atakuwa Nashoni mwana wa Aminadabu.

4. Na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa sabini na nne elfu na mia sita.

5. Na hao watakaopanga karibu naye ni kabila ya Isakari; na mkuu wa wana wa Isakari atakuwa Nethaneli mwana wa Suari;

6. na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa hamsini na nne elfu na mia nne;

7. na kabila ya Zabuloni; na mkuu wa wana wa Zabuloni atakuwa Eliabu mwana wa Heloni;

8. na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa hamsini na saba elfu na mia nne.

Hes. 2