Hes. 17:11-13 Swahili Union Version (SUV)

11. Basi Musa akafanya vivyo; kama BWANA alivyomwagiza, ndivyo alivyofanya.

12. Kisha wana wa Israeli wakanena na Musa, na kumwambia, Angalia, sisi twafa, twaangamia, sote twaangamia.

13. Kila mtu akaribiaye, aikaribiaye maskani ya BWANA, hufa; je! Tutakufa pia sote?

Hes. 17