Hes. 14:33-43 Swahili Union Version (SUV)

33. Kisha watoto wenu watakuwa wachungaji jangwani muda wa miaka arobaini nao watauchukua mzigo wa uasherati wenu, hata mizoga yenu itakapoangamia jangwani.

34. Kwa hesabu ya hizo siku mlizoipeleleza ile nchi, yaani, siku arobaini kila siku kuhesabiwa mwaka, mtayachukua maovu yenu, ndiyo miaka arobaini, nanyi mtakujua kufarikana kwangu.

35. Mimi BWANA nimekwisha nena, hakika yangu ndilo nitakaloutenda mkutano mwovu huu wote, waliokusanyika juu yangu; wataangamia katika nyika hii, nako ndiko Watakakokufa.

36. Kisha hao watu, ambao Musa aliwatuma waipeleleze nchi, waliorudi, na kufanya mkutano wote kumnung’unikia, kwa walivyoleta habari mbaya juu ya nchi,

37. watu hao walioileta habari mbaya ya nchi wakafa kwa tauni mbele ya BWANA.

38. Lakini Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, wakabaki hai miongoni mwa wale watu waliokwenda kuipeleleza nchi.

39. Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli wote maneno haya, na hao watu wakaombolea sana.

40. Wakainuka na mapema asubuhi, wakakwea juu ya mlima hata kileleni, wakisema, Tazameni, sisi tupo hapa, nasi tutakwea kwenda mahali BWANA alipotuahidi; kwani tumefanya dhambi.

41. Musa akawaambia, Kwa nini ninyi sasa kuyahalifu maagizo ya BWANA? Maana halitafanikiwa jambo hilo.

42. Msikwee, kwa kuwa BWANA hamo kati yenu; msipigwe na kuangushwa mbele ya adui zenu.

43. Kwa kuwa Mwamaleki na Mkanaani wako mbele yenu, nanyi mtaanguka kwa upanga, kwa sababu mmerudi nyuma msimwandame BWANA, kwa hiyo BWANA hatakuwa pamoja nanyi.

Hes. 14