Hes. 13:4-20 Swahili Union Version (SUV)

4. Na majina yao ni haya; katika kabila ya Reubeni, Shamua mwana Zakuri.

5. Katika kabila ya Simeoni, Shafati mwana wa Hori.

6. Katika kabila ya Yuda, Kalebu mwana wa Yefune.

7. Katika kabila ya Isakari, Igali mwana wa Yusufu.

8. Katika kabila ya Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni

9. Katika kabila ya Benyamini, Palti mwana wa Rafu.

10. Katika kabila ya Zabuloni, Gadieli mwana wa Sodi.

11. Katika kabila ya Yusufu, yaani, katika kabila ya Manase, Gadi mwana wa Susi.

12. Katika kabila ya Dani, Amieli mwana wa Gemali.

13. Katika kabila ya Asheri, Sethuri mwana wa Mikaeli.

14. Katika kabila ya Naftali, Nabi mwana wa Wofsi.

15. Katika kabila ya Gadi, Geueli mwana wa Maki.

16. Hayo ndiyo majina ya hao watu waliotumwa na Musa waende kuipeleleza nchi. Na huyo Hoshea mwana wa Nuni, Musa akamwita jina lake Yoshua.

17. Musa akawapeleka ili waipeleleze nchi ya Kanaani, akawaambia, Pandeni sasa katika Negebu mkapande milimani,

18. mkaitazame nchi ni ya namna gani; na watu wanaokaa ndani yake, kwamba ni hodari au dhaifu, kwamba ni wachache au wengi;

19. na nchi wanayoikaa kwamba ni njema au mbaya; kwamba wanakaa katika matuo au katika ngome;

20. nayo nchi ni ya namna gani, kwamba ni nchi ya unono au ya njaa, kwamba ina msitu au sivyo. Iweni na moyo mkuu, mkayalete matunda ya nchi. Basi wakati ule ulikuwa wakati wa kuiva zabibu za kwanza.

Hes. 13