Hes. 11:1-2 Swahili Union Version (SUV)

1. Kisha hao watu walikuwa kama wanung’unikao, wakinena maovu masikioni mwa BWANA; BWANA aliposikia hayo, hasira zake zikawaka; na moto wa BWANA ukawaka kati yao, ukateketeza katika mipaka ya mwisho wa marago.

2. Ndipo watu wakamlilia Musa; naye Musa akamwomba BWANA, na ule moto ukakoma.

Hes. 11