10. Katika wana wa Yusufu; wa Efraimu, Elishama mwana wa Amihudi; na wa Manase; Gamalieli mwana wa Pedasuri.
11. Wa Benyamini Abidani mwana wa Gideoni.
12. Wa Dani; Ahiezeri mwana wa Amishadai.
13. Wa Asheri; Pagieli mwana wa Okirani.
14. Wa Gadi; Eliasafu mwana wa Deueli.
15. Wa Naftali; Ahira mwana wa Enani.
16. Hao ndio walioitwa wa mkutano, wakuu wa kabila za baba zao; nao ndio vichwa vya wale maelfu ya Israeli.
17. Basi Musa na Haruni wakawatwaa hao watu waume waliotajwa majina yao;
18. nao waliukutanisha mkutano mzima, siku ya kwanza ya mwezi wa pili, nao wakaonyesha ukoo wa vizazi vyao kwa kuandama jamaa zao, kwa nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, tangu umri wa miaka ishirini na zaidi, kichwa kwa kichwa.
19. Kama BWANA alivyomwagiza Musa, ndivyo alivyowahesabu huko katika bara ya Sinai.