Hes. 1:1-14 Swahili Union Version (SUV)

1. BWANA akanena na Musa katika bara ya Sinai, hemani mwa kukutania, siku ya kwanza ya mwezi wa pili, katika mwaka wa pili baada ya kutoka kwao nchi ya Misri, akamwambia,

2. Fanyeni hesabu ya mkutano wote wa wana wa Israeli, kwa kuandama jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina ilivyo, kila mtu mume kichwa kwa kichwa;

3. tangu mwenye miaka ishirini umri wake, na zaidi, wote wawezao kutoka kwenenda vitani katika Israeli; wewe na Haruni mtawahesabu kwa kuandama majeshi yao.

4. Tena mtu mume mmoja wa kila kabila atakuwa pamoja nanyi; kila mmoja aliye kichwa cha nyumba ya baba zake.

5. Na majina ya hao waume watakaosimama pamoja nanyi ni haya; Wa Reubeni; Elisuri mwana wa Shedeuri.

6. Wa Simeoni; Shelumieli mwana wa Suri-shadai.

7. Wa Yuda; Nashoni mwana wa Aminadabu.

8. Wa Isakari; Nethaneli mwana wa Suari.

9. Wa Zabuloni; Eliabu mwana wa Heloni.

10. Katika wana wa Yusufu; wa Efraimu, Elishama mwana wa Amihudi; na wa Manase; Gamalieli mwana wa Pedasuri.

11. Wa Benyamini Abidani mwana wa Gideoni.

12. Wa Dani; Ahiezeri mwana wa Amishadai.

13. Wa Asheri; Pagieli mwana wa Okirani.

14. Wa Gadi; Eliasafu mwana wa Deueli.

Hes. 1