Hab. 3:9-14 Swahili Union Version (SUV)

9. Uta wako ukafanywa wazi kabisa;Viapo walivyopewa kabila vilikuwa neno thabiti;Ukaipasua nchi kwa mito.

10. Milima ilikuona, ikaogopa;Gharika ya maji ikapita;Vilindi vikatoa sauti yake,Vikainua juu mikono yake.

11. Jua na mwezi vikasimama makaoni mwao;Mbele ya nuru ya mishale yako ilipotapakaa,Mbele ya mwangaza wa mkuki wako umeremetao.

12. Ulikwenda katikati ya nchi kwa ghadhabu;Ukawapura mataifa kwa hasira.

13. Ukatokea kwa ajili ya wokovu wa watu wako,Kwa ajili ya wokovu wa masihi wako;Ukakiponda kichwa cha nyumba ya waovu,Ukiuweka wazi msingi hata mwambani.

14. Ukakichoma kichwa cha mashujaa wake kwa fimbo zao wenyewe;Wakaja kama kisulisuli ili kunitawanya;Kama wakifurahi kuwameza maskini kwa siri.

Hab. 3