Hab. 3:14-19 Swahili Union Version (SUV)

14. Ukakichoma kichwa cha mashujaa wake kwa fimbo zao wenyewe;Wakaja kama kisulisuli ili kunitawanya;Kama wakifurahi kuwameza maskini kwa siri.

15. Ukaikanyaga bahari kwa farasi zako,Chungu ya maji yenye nguvu.

16. Nikasikia, na tumbo langu likatetemeka,Midomo yangu ikatikisika kwa sauti ile;Ubovu ukaingia mifupani mwangu,Nikatetemeka katika mahali pangu;Ili nipate kuingoja ile siku ya dhiki,Kundi lao washambuliao wakweapo juu ya watu.

17. Maana mtini hautachanua maua,Wala mizabibuni hamtakuwa na matunda;Taabu ya mzeituni itakuwa bure,Na mashamba hayatatoa chakula;Zizini hamtakuwa na kundi,Wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng’ombe;

18. Walakini nitamfurahia BWANANitamshangilia Mungu wa wokovu wangu.

19. YEHOVA, aliye BWANA, ni nguvu zangu,Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu,Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.

Hab. 3