Gal. 5:8-16 Swahili Union Version (SUV)

8. Kushawishi huku hakukutoka kwake yeye anayewaita ninyi.

9. Chachu kidogo huchachua donge zima.

10. Nina matumaini kwenu katika Bwana, ya kwamba hamtakuwa na nia ya namna nyingine. Lakini yeye anayewafadhaisha atachukua hukumu yake, awaye yote.

11. Nami, ndugu zangu ikiwa ninahubiri habari ya kutahiriwa, kwa nini ningali ninaudhiwa? Hapo kwazo la msalaba limebatilika!

12. Laiti hao wanaowatia mashaka wangejikata nafsi zao!

13. Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.

14. Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako.

15. Lakini mkiumana na kulana, angalieni msije mkaangamizana.

16. Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.

Gal. 5