Gal. 5:16-20 Swahili Union Version (SUV)

16. Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.

17. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.

18. Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.

19. Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,

20. ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,

Gal. 5