Gal. 5:1-7 Swahili Union Version (SUV)

1. Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.

2. Tazama, mimi Paulo nawaambia ninyi ya kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidia neno.

3. Tena namshuhudia kila mtu atahiriwaye, kwamba ni wajibu wake kuitimiza torati yote.

4. Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema.

5. Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani.

6. Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.

7. Mlikuwa mkipiga mbio vizuri; ni nani aliyewazuia msiitii kweli?

Gal. 5