Gal. 4:27-31 Swahili Union Version (SUV)

27. Kwa maana imeandikwa,Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa;Paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu;Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengiKuliko wa huyo aliye na mume.

28. Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi.

29. Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo na sasa.

30. Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana.

31. Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, bali tu watoto wa huyo aliye mwungwana.

Gal. 4