1. Paulo, mtume, (si mtume wa wanadamu, wala kutumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu),
2. na ndugu wote walio pamoja nami, kwa makanisa ya Galatia;
3. Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba, na kwa Bwana wetu Yesu Kristo;
4. ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu, ili atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu.
5. Utukufu una yeye milele na milele, Amina.
6. Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine.
7. Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo.