18. Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu.
19. Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.
20. Sasa atukuzwe Mungu, Baba yetu, milele na milele. Amina.
21. Mnisalimie kila mtakatifu katika Kristo Yesu. Ndugu walio pamoja nami wawasalimu.
22. Watakatifu wote wawasalimu, hasa wao walio wa nyumbani mwa Kaisari.
23. Neema ya Bwana Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu.