Flp. 4:13-17 Swahili Union Version (SUV)

13. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

14. Lakini mlifanya vema, mliposhiriki nami katika dhiki yangu.

15. Nanyi pia, ninyi wenyewe mnajua, enyi Wafilipi, ya kuwa katika mwanzo wa Injili, nilipotoka Makedonia, hakuna kanisa lingine lililoshirikiana nami katika habari hii ya kutoa na kupokea, ila ninyi peke yenu.

16. Kwa kuwa hata huko Thesalonike mliniletea msaada kwa mahitaji yangu, wala si mara moja.

17. Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu.

Flp. 4