Flp. 1:1-6 Swahili Union Version (SUV)

1. Paulo na Timotheo, watumwa wa Kristo Yesu, kwa watakatifu wote katika Kristo Yesu, walioko Filipi, pamoja na maaskofu na mashemasi.

2. Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.

3. Namshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo,

4. sikuzote kila niwaombeapo ninyi nyote nikisema sala zangu kwa furaha,

5. kwa sababu ya ushirika wenu katika kuieneza Injili, tangu siku ile ya kwanza hata leo hivi.

6. Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;

Flp. 1