Flm. 1:13-25 Swahili Union Version (SUV)

13. ambaye mimi nalitaka akae kwangu, apate kunitumikia badala yako katika vifungo vya Injili.

14. Lakini sikutaka kutenda neno lo lote isipokuwa kwa shauri lako, ili kwamba wema wako usiwe kama kwa lazima, bali kwa hiari.

15. Maana, labda ndiyo sababu alitengwa nawe kwa muda, ili uwe naye tena milele;

16. tokea sasa, si kama mtumwa, bali zaidi ya mtumwa, ndugu mpendwa; kwangu mimi sana, na kwako wewe zaidi sana, katika mwili na katika Bwana.

17. Basi kama ukiniona mimi kuwa mshirika nawe, mpokee huyu kama mimi mwenyewe.

18. Na kama amekudhulumu, au unamwia kitu, ukiandike hicho juu yangu.

19. Mimi Paulo nimeandika kwa mkono wangu mwenyewe, mimi nitalipa. Sikuambii kwamba nakuwia hata nafsi yako.

20. Naam, ndugu yangu, nipate faida kwako katika Bwana; uniburudishe moyo wangu katika Kristo.

21. Kwa kuwa nakuamini kutii kwako ndiyo maana nimekuandikia, nikijua ya kuwa utafanya zaidi ya hayo nisemayo.

22. Na pamoja na hayo uniwekee tayari mahali pa kukaa; maana nataraji ya kwamba kwa maombi yenu mtajaliwa kunipata.

23. Epafra, aliyefungwa pamoja nami katika Kristo Yesu, akusalimu;

24. na Marko, na Aristarko, na Dema, na Luka, watendao kazi pamoja nami.

25. Neema ya Bwana Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu.

Flm. 1