Ezr. 2:69-70 Swahili Union Version (SUV)

69. wakatoa kadiri walivyoweza, na kutia katika hazina ya kazi hiyo, darkoni za dhahabu sitini na moja elfu, na mane za fedha elfu tano, na mavazi mia ya makuhani.

70. Hivyo makuhani, na Walawi, na baadhi ya watu, na waimbaji, na mabawabu, na Wanethini, wakakaa mijini mwao, naam, Israeli wote wakakaa mijini mwao.

Ezr. 2