30. Watu wa Magbishi, mia moja hamsini na sita.
31. Watu wa Elamu wa pili, elfu moja mia mbili hamsini na wanne.
32. Watu wa Harimu, mia tatu na ishirini.
33. Watu wa Lodi, na Hadidi, na Ono, mia saba ishirini na watano.
34. Watu wa Yeriko, mia tatu arobaini na watano.
35. Watu wa Senaa, elfu tatu mia sita na thelathini.
36. Makuhani; wana wa Yedaya, wa mbari ya Yeshua, mia kenda sabini na watatu.
37. Wana wa Imeri, elfu moja hamsini na wawili.
38. Wana wa Pashuri, elfu moja mia mbili arobaini na saba.
39. Wana wa Harimu, elfu moja na kumi na saba.
40. Walawi; wana wa Yeshua, na wana wa Kadmieli wa wana wa Hodavia, sabini na wanne.
41. Waimbaji; wana wa Asafu, mia moja ishirini na wanane.
42. Akina bawabu; wana wa Shalumu, wana wa Ateri, wana wa Talmoni, wana wa Akubu, wana wa Hatita, wana wa Shobai; jumla yao ni mia moja thelathini na kenda.
43. Wanethini; wana wa Siha, wana wa Hasufa, wana wa Tabaothi;