15. Wana wa Adini, mia nne hamsini na wanne.
16. Wana wa Ateri, wa wana wa Hezekia, tisini na wanane.
17. Wana wa Besai, mia tatu ishirini na watatu.
18. Wana wa Harifu, mia moja na kumi na wawili.
19. Wana wa Hashumu, mia mbili ishirini na watatu.
20. Watu wa Gibeoni, tisini na watano.
21. Watu wa Bethlehemu, mia ishirini na watatu.
22. Watu wa Netofa, hamsini na sita.
23. Watu wa Anathothi, mia ishirini na wanane.
24. Watu wa Beth-Azmawethi, arobaini na wawili.
25. Watu wa Kiriath-yearimu, na Kefira, na Beerothi, mia saba arobaini na watatu.
26. Watu wa Rama na Geba, mia sita ishirini na mmoja.
27. Watu wa Mikmashi, mia moja ishirini na wawili.