Nami nitapeleka juu yenu njaa na wanyama wabaya, nao watakunyang’anya watu wako; na tauni na damu zitapita ndani yako; nami nitauleta upanga juu yako; mimi BWANA, nimeyanena hayo.