1. Kisha akanirudisha kwa njia ya lango lile la nje, la mahali patakatifu lililoelekea upande wa mashariki; nalo lilikuwa limefungwa.
2. BWANA akaniambia, Lango hili litafungwa, halitafunguliwa, wala mtu awaye yote hataingia kwa lango hili, kwa maana BWANA, Mungu wa Israeli, ameingia kwa hilo; basi kwa sababu hiyo litafungwa.
3. Na mkuu, yeye ndiye atakayeketi ndani yake ale chakula mbele za BWANA; ataingia kwa njia ya ukumbi wa lango, naye atatoka kwa njia iyo hiyo.