Eze. 35:1-5 Swahili Union Version (SUV)

1. Tena neno la BWANA likanijia, kusema,

2. Mwanadamu, kaza uso wako juu ya mlima Seiri, ukatabiri juu yake,

3. uuambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ee mlima Seiri, nami nitaunyosha mkono wangu juu yako, nami nitakufanya kuwa ukiwa na ajabu.

4. Miji yako nitaiharibu, nawe utakuwa ukiwa; nawe utajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.

5. Kwa kuwa umekuwa na uadui usiokoma, nawe umewatoa wana wa Israeli wapigwe kwa nguvu za upanga, wakati wa msiba wao, wakati wa mwisho wa uovu.

Eze. 35