Eze. 18:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Neno la BWANA likanijia tena, kusema,

2. Je! Maana yake ni nini hata mkatumia mithali hii katika Israeli, mkisema, Baba wamekula zabibu mbichi, nao watoto wakatiwa ganzi la meno?

3. Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hamtakuwa na sababu ya kuitumia tena mithali hii katika Israeli.

Eze. 18