Eze. 11:22-25 Swahili Union Version (SUV)

22. Ndipo hao makerubi wakainua mabawa yao, nayo magurudumu yalikuwa karibu nao, nao utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao.

23. Utukufu wa BWANA ukapaa juu toka katikati ya mji, ukasimama juu ya mlima wa upande wa mashariki wa mji.

24. Na roho hiyo ikaniinua, ikanichukua katika maono, kwa nguvu za roho ya Mungu, hata Ukaldayo, kwa watu wale wa uhamisho. Basi maono niliyoyaona yakaniacha.

25. Ndipo nikawaambia watu wa uhamisho habari ya mambo yote aliyonionyesha BWANA.

Eze. 11