Est. 4:15-17 Swahili Union Version (SUV)

15. Basi Esta akawatuma ili wamjibu Mordekai,

16. Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie.

17. Basi Mordekai akaenda zake, akafanya yote kama vile Esta alivyomwagiza.

Est. 4