Efe. 5:5-21 Swahili Union Version (SUV)

5. Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.

6. Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi.

7. Basi msishirikiane nao.

8. Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru,

9. kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli;

10. mkihakiki ni nini impendezayo Bwana.

11. Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee;

12. kwa kuwa yanayotendeka kwao kwa siri, ni aibu hata kuyanena.

13. Lakini yote yaliyokemewa hudhihirishwa na nuru maana kila kilichodhihirika ni nuru.

14. Hivyo husema,Amka, wewe usinziaye,Ufufuke katika wafu,Na Kristo atakuangaza.

15. Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;

16. mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.

17. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.

18. Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;

19. mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu;

20. na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;

21. hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo.

Efe. 5