Efe. 5:10-24 Swahili Union Version (SUV)

10. mkihakiki ni nini impendezayo Bwana.

11. Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee;

12. kwa kuwa yanayotendeka kwao kwa siri, ni aibu hata kuyanena.

13. Lakini yote yaliyokemewa hudhihirishwa na nuru maana kila kilichodhihirika ni nuru.

14. Hivyo husema,Amka, wewe usinziaye,Ufufuke katika wafu,Na Kristo atakuangaza.

15. Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;

16. mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.

17. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.

18. Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;

19. mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu;

20. na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;

21. hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo.

22. Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.

23. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.

24. Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.

Efe. 5