Efe. 4:1-10 Swahili Union Version (SUV)

1. Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa;

2. kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo;

3. na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani.

4. Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.

5. Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja.

6. Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.

7. Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo.

8. Hivyo husema,Alipopaa juu aliteka mateka,Akawapa wanadamu vipawa.

9. Basi neno hilo, Alipaa, maana yake nini kama siyo kusema kwamba yeye naye alishuka mpaka pande zilizo chini za nchi?

10. Naye aliyeshuka ndiye yeye aliyepaa juu sana kupita mbingu zote, ili avijaze vitu vyote.

Efe. 4