Ebr. 9:1-5 Swahili Union Version (SUV)

1. Basi hata agano la kwanza lilikuwa na kawaida za ibada, na patakatifu pake, pa kidunia.

2. Maana hema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na kinara cha taa, na meza, na mikate ya Wonyesho; ndipo palipoitwa, Patakatifu.

3. Na nyuma ya pazia la pili, ile hema iitwayo Patakatifu pa patakatifu,

4. yenye chetezo cha dhahabu, na sanduku la agano lililofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye ile mana, na ile fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vile vibao vya agano;

5. na juu yake makerubi ya utukufu, yakikitia kivuli kiti cha rehema; basi hatuna nafasi sasa ya kueleza habari za vitu hivi kimoja kimoja.

Ebr. 9