Ebr. 7:18-25 Swahili Union Version (SUV)

18. Maana, kuna kubatiliwa kwa ile amri iliyotangulia, kwa sababu ya udhaifu wake, na kutokufaa kwake;

19. (kwa maana ile sheria haikukamilisha neno); na pamoja na hayo kuliingizwa matumaini yaliyo mazuri zaidi, ambayo kwa hayo twamkaribia Mungu.

20. Na kwa kuwa haikuwa pasipo kiapo,

21. (maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; bali yeye, pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia,Bwana ameapa wala hataghairi,Wewe u kuhani milele;)

22. basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi.

23. Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu wazuiliwa na mauti wasikae;

24. bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.

25. Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.

Ebr. 7