Ebr. 7:16-22 Swahili Union Version (SUV)

16. asiyekuwa kuhani kwa sheria ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na ukomo;

17. maana ameshuhudiwa kwamba,Wewe u kuhani mileleKwa mfano wa Melkizedeki.

18. Maana, kuna kubatiliwa kwa ile amri iliyotangulia, kwa sababu ya udhaifu wake, na kutokufaa kwake;

19. (kwa maana ile sheria haikukamilisha neno); na pamoja na hayo kuliingizwa matumaini yaliyo mazuri zaidi, ambayo kwa hayo twamkaribia Mungu.

20. Na kwa kuwa haikuwa pasipo kiapo,

21. (maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; bali yeye, pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia,Bwana ameapa wala hataghairi,Wewe u kuhani milele;)

22. basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi.

Ebr. 7