5. Na Musa kweli alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa baadaye;
6. bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba ya Mungu; ambaye nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na fahari ya taraja letu mpaka mwisho.
7. Kwa hiyo, kama anenavyo Roho Mtakatifu,Leo, kama mtaisikia sauti yake,
8. Msifanye migumu mioyo yenu,Kama wakati wa kukasirisha,Siku ya kujaribiwa katika jangwa,
9. Hapo baba zenu waliponijaribu, wakanipima,Wakaona matendo yangu miaka arobaini.
10. Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki,Nikasema, Sikuzote ni watu waliopotoka mioyo hawa;Hawakuzijua njia zangu;
11. Kama nilivyoapa kwa hasira yangu,Hawataingia rahani mwangu.
12. Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hai.
13. Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.
14. Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho;