7. Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni imani yao.
8. Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele.
9. Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo hawakupata faida.
10. Tuna madhabahu ambayo wale waihudumiao ile hema hawana ruhusa kula vitu vyake.