9. Umependa haki, umechukia maasi;Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta,Mafuta ya shangwe kupita wenzio.
10. Na tena,Wewe, Bwana, hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi,Na mbingu ni kazi za mikono yako;
11. Hizo zitaharibika, bali wewe unadumu;Nazo zote zitachakaa kama nguo,
12. Na kama mavazi utazizinga, nazo zitabadilika;Lakini wewe u yeye yule,Na miaka yako haitakoma.
13. Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote,Uketi mkono wangu wa kuumeHata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako?